Siku ya Jumamosi ya tarehe 6 mwezi tatu, Kampuni inayojihusisha na Blockchain, Jelurida Africa, ilifanikiwa kufanya mkutano wake wa kwanza kabisa nchini Tanzania. Mkutano huo ambao ulikuwa unajadili masuala ya vitu visivyohamishika, ulikuwa ni mmoja kati ya mikutano mingi ambayo kampuni inapanga kuifanya ndani ya mwaka huu ikiwaa ni katika maandilizi ya mipango mikuu ambao ni Ulaya na africa blockchain “developer”.
Kikao hiki kilikuwa ni cha kukutana lakini pia kwa njia ya mtandao. waakiokutana walikuwa katika chuo cha PSJ (Practical School of Journalism) ambacho kipo Dar Es Salaam, wanafunzi mbali mbali, wapenda blockchain mbalimbali na watu mbali mbali walihudhuria.Mkutano uliendeshwa na muwakilishi wa kampuni nchini Tanzania ndugu Charles Chale na ulirushwa moja kwa moja ili watu walio maeneo ya mbali na nchi mbali mbali waweze kujumuika.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jelurida Afrika, Adebayo Adebajo, alifundisha kwa kutumia njia ya mtandao jinsi Blockchain inavyoweza kutumika katika sekta ya biashara ya mali zisizohamishika na pia alijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa baada ya kufundisha.

Mbali na mkurugenzi mtendaji wa kampuni wakufunzi mbali mbali kutoka vyuo mbalimbali nchini walihudhuria kikao. Wakufunzi kutoka chuo cha mtakatifu agustino (St. Augustine University), Chuo cha mtakatifu John (St.John University) na chuo cha Mzumbe ( Mzumbe University) vyote vya nchini Tanzania.Kuweza kuangalia video ya kikao kilichofanyika Tafadhali tembelea https://youtu.be/ZYUN3klrRAg.