skip to Main Content

Bitcoin, Cryptocurrency-Maana Na Jinsi Inavyofanya Kazi

Bitcoin

Sehemu ya kwanza

Miaka kuku na moja iliyopita, neno “cryptocurrency”lilionekana la ajabu kwa wengi. Hata Sasa hili neno limekuwa likisikika mara kwa mara lakini bado watu wengi wamekuwa hawajui linamaanisha nini hasa. Ni neno lililozoeleka Kama fedha za mtandaoni ama Bitcoin.

Je fedha za mtandaoni ni nini hasa?

Watu wengi Wana uelewa potofu juu ya fedha za mtandaoni, kwa baadhi ni neno linalohusishwa na wizi na njia zisizo halali za kifedha, kwa wengine hili neno limekuwa msamiati watu wakitumia kutengeneza fedha. Cryptocurrencies inaweza kuelezewa na kueleweka kwa njia rahisi. Uelewa wa mahesabu yake huchukua mda mrefu Sana. Ingawa, kuwa na uelewa kidogo juu ya mfumo wa thamani yake Ni kitu pekee kinachohitajika ili uweze kutumia.

Je Cryptocurrency ni nini?

Cryptocurrency ni fedha ya kimtandao iliyo dhahiri au halisi ambayo inaweza kutumika kubadilishana au kufanya manunuzi. Inaweza kuonekana Kama fedha ya kawaida, lakini ambayo mtu hawezi kushika. Ili kupata uelewa sahihi wa dhana hii,uione kama hawala ya fedha-naira ya Nigeria, Cedi ya Ghana, dola ya Marekani,Shilingi ya Kenya au Rand ya Afrika kusini. Cryptocurrencies inafanyanishwa na aina hizi za hawala, lakini ikiwa na tofauti kuu-cryptocurrency ni ya uhalisia.

Tofauti na hawala ya kawaida, Cryptocurrencies hazimilikiwi na eneo ama nchi Fulani, kwahiyo zenyewe zinaweza kutumiwa na mtu yeyote, popote (Ingawa, uhalalishaji wake ni hafifu kwa baadhi ya nchi).

Kitu gani kinafanya ziwe salama?

Cryptocurrencies zinadhibitiwa na fumbo (cryptography). Fumbo Ni njia ya kulinda ujumbe ndani ya mtandao. Katika kipindi ambacho biashara nyingi na miamala mingi imehamia katika mfumo wa digit, fumbo (cryptography) inabeba jukumu muhimu ya kulinda taarifa ambazo zinakuwa zinabadilishwa katika tovuti mbalimbali duniani. Fumbo inafumba taarifa au jumbe ili iweze kumfikia muhusika pekee (mlengwa). Cha kushangaza fumbo haikuanzia kwenye mitandao. Ni mfumo ulioanza kutumika tangu miaka ya 1900 Kabla ya Kristo.

Jinsi gani mfumo wa fumbo (cryptography) unavyofanya kazi na fedha za mtandaoni.

Kitu cha muhimu katika mfumo wa fumbo kwenye nadharia ya fedha za mtandao ni suala la saini ya digiti. Saini mara nyingi inatumika kuonesha uhalali katika dunia ya mtandao na vivyo hivyo ndivyo inavyotumika katika ulimwengu wa digiti. Saini itakuonesha mmiliki wa hati, hakitakiwi ighushike, na pindi hati ikisainiwa saini haiwezi kuondolewa. Hivi ndivyo saini za kidigiti hufanya.

Hata hivyo, japokuwa saini ni njia Bora ya kuonesha uhalali, bado zinaweza kughushika. Ili kuondokana na changamoto hii, mfumo wa fumbo unaenda hatua moja zaidi kwa kuongeza funguo katika sahihi hizi za kidigiti. Funguo hizi zinafunga hati ili kuhakikisha macho yanayochungulia kushindwa kuona sahihi. 

Kuna mahesabu magumu mno katika mfumo wa fumbo ambazo zinasaidia katika fedha za mtandao hivyo huzifanya fedha hizo kutumika kwa ufasaha.

Historia fupi ya Bitcoin na fedha za mtandao

Flooz, Beenz na DigiCash ni Kati ya walionza mapema kutumia fedha za mtandaoni mnamo miaka ya 90, kwa bahati mbaya wote walishindwa. Kwa matokeo hayo, kushindwa kwa majaribio yao ya kwanza kuhusu fedha za kidigitali, kulifanya wazo zima kupoteza muelekeo na hakukuwa na kumbukumbu ya majaribio yaliyorekodiwa tena tangu kipindi hiko.

Kisha akaja Satoshi mwaka 2009 mtaalamu wa kompyuta asiyejulikana, aliyetumia jina la Satochi Nakamoto, alikuja na wazo la Bitcoin. Alielezea Bitcoin kuwa haipo chini ya mamlaka yeyote ambayo haikuhitaji mtu yeyote wa katikati. Kutuma fedha ilikuwa rahisi Kama kutuma faili kutoka kwenye simu moja kwenda kwemye simu nyingine.

Hali ya fedha ya mtandaoni kutokuwa chini ya mamlaka yeyote ni moja ya sifa yake bora zaidi. Kama ilivyo aina ya Mitandao mingine ya malipo ilitakiwa ishughulikie tatizo la kulipia kitu mara mbili. Kulipia Mara mbili ni kitendo Cha kitapeli Cha kutumia kiasi kile kile Cha fedha Mara mbili. Njia ya kawaida ya kutatua tatizo hili ni kwa kutengeneza mfumo ambao utatunza rekodi ya kila muamala na kumbukumbu ya salio. Hata hivyo, mfumo hu unahitaji mtu wa tatu ambaye atakuwa na taarifa sahihi baina ya watumiaji wawili. Bitcoin za Satoshi zinahitaji sehemu maalumu ha kutunzia kumbukumbu. Inatumia mfumo wa kutunza kumbukumbu ambao umetawanywa unaojulikana kama blockchain. Hii inaondoa haha ya kuwa na mfumo mmoja wa kuhifadhia kumbukumbu za miamala. Blockchain ni mfumo wa kumbukumbu ambao unaacha nakala ya kumbukumbu kwa kila mtumiaji. Mabadiliko yeyote yanayofanywa katika mfumo huu huweka kumbukumbu hiyo kwenye nakala ya watu wote, hivyo basi kufanya mtu mmojawapo asiweze kubadilisha taarifa kwenye kila kumbukumbu.

Ndani ya mtandao wa fedha za kimtandao kama Bitcoin, watumiaji wanathibitisha mialama. Watumiaji wanafanya hivi kwa kutatua mfumo mgumu uliowekwa.

Kwahiyo, namna gani tunaweza kutumia fedha za mtandao?

Kama fedha nyingine,fedha ya mtandao inaweza kutumika kulipia bidhaa na huduma. Mnamo tarehe 22 mwezi wa tano mwaka 2010, mwanamme mmoja kwa jina la Lazlo Hanyecza alilipia pizza yake kwa Bitcoin 10,000. Hii ilikuwa Mara ya kwanza kwa fedha ya mtandaoni kutumika Kama njia ya kufanya manunuzi. Hii siku inajulikana Kama siku ya Bitcoin pizza. Leo, Lazlo angelipia dola 231,000 kwa ajili ya hiyo pizza.

Kuna wafanyabiashara wengi ambao wangekubali fedha za mtandaoni Kama malipo. Katika maduka ya apple, fedha ya mtandaoni imethibitishwa Kama njia ya malipo. Katika maeneo mengi ya Afrika Kama vile Nigeria, Ni njia Bora ya kufanya malipo nje ya mipaka.

Ukiachana kutumika Kama njia ya malipo ,fedha za mtandaoni pia zinatumika Kama njia mojawapo ya uwekezaji. Mtu ambaye aliwekeza Bitcoin moja mwaka 2010, kipindi ambacho Bitcoin ilikuwa chini ya dola moja, angeweza kupata $ 18,000.

Ingawa Bitcoin inaweza kuwa Kati ya vitu vya thamani ndani ya miaka kumi ni muhimu kujua kwamba fedha za mtandao zinabadilika haraka Sana, hivyo kufanya uwekezaji wake uwe wa hatari.

Bitcoin, fedha ya mtandaoni iliyo imara zaidi ilishuka kwa ghafla Sana mwaka 2017. Thamani yake ilipanda Sana hadi $20,000 na ikashuka ghafla Hadi $3000. Hata hivyo, fedha hii imeendelea kupanda juu Sana. Kwa Sasa ina thamani ya $23,000 wakati wa kuandika makala hii.

Ushuhuda kutoka kwenye kazi za uvunaji

Fedha za mtandaoni pia zinaweza zikavunwa. Uvunaji ni muhimu Sana kwa fedha za mtandaoni, hasa kwa wale wanaotumia mfumo wa POW. Wavunaji wanathibitisha muamala ili iweze kuwekwa katika kumbukumbu. Kwa kufanya hivyo, wanaongeza huduma za utunzaji taarifa za miamala. Wavunaji wanatatua mafumbo mbalimbali ya fedha za mtandaoni. Mafumbo yanazidi kuwa magumu kwa fedha maarufu kadri siku zinavyozidi kwenda. Siku hizi mahesabu ya Hali ya juu mno yanahitajika ili mtu aweze kufanikiwa kuvuna. Kwa kila fumbo litakalotatuliwa mvunaji anapewa zawadi ya Bitcoin. Uvunaji ni kati ya njia inayoifanya sarafu kuzunguka. Miaka inavyozidi kwenda kiwango Cha zawadi kwa wavunaji kimekuwa kikipunguzwa ili kupunguza mzunguko wa fedha za mtandaoni. Hii pia imekuwa sababu ya Bitcoin kuongezeka thamani. Wavunaji walikuwa wanapewa zawadi ya Bitcoin 50 hawati fedha hii inaanza, Sasa hivi zawadi Ni Bitcoin 6.25. Hata hivyo zawadi hii itaendelea kushika mda unavyozidi kwenda. Bitcoin milioni mbili tu ndizo zilizobaki kuvunwa. Kuvunwa kwa hizo kutafanya kuwe na na Bitcoin milioni 21 katika mzunguko.

Uwekaji wa dau uhitaji waweka dau wabainishe kiasi Cha dau.

Ukiacha uvunaji, fedha nyingine zinatumia mfumo wa dau. Bitcoin inahitaji mvunaji kuthibitisha muamala, frledha nyingine za mtandao hazihitaji hivyo. Mfano Ni ethereum 2.0, fedha hii ikiwa ni ya pili kwa ukubwa ukiacha bitcoin. Ethereum inahitaji kuthibitisha muamala unaotokea ndani ya mtandao wa ethereum. Wahakiki wanahitaji dau la angalau ethereum 32 ili kukupa haki ya kuhakiki.

Uhakiki hatuhitaji mahesabu ya Hali ya juu Kama uvunaji. Kompyuta ya kawaida inaweza kuhakiki.

Uwekaji wa dau, hata hivyo haujaanza bado kutumika katika mtandao wa ethereum. Ni mfumo mpya ndani ya mtay ambao utaanza kutumika mnamo mwaka 2021.

Kujifunza kuhusu fedha za mtandao ni hatua ambayo inaanza kwa kuzimiliki kwanza. Kusoma maoni katika mitandao ya kijamii kutachangia uelewa zaidi. Fuatilia akaunti mbalimbali za mitandao ya kijamii na taarifa mbalimbali ili kufanya maamuzi sahihi kwenye fedha za mtandao

Comments

Decentralize Daily

From Crypto and Blockchain to AI, Fintech and Web 3.0 delivered twice in a week (Mondays and Fridays)

Latest Articles
Subscribe To Our Newsletter

Don't get left out of the loop, make sure you subscribe to our newsletter below so you can be notified of our latest insights, tips, tutorials, sales and more!

Discussion

This Post Has 0 Comments

Leave a comment:

Back To Top
%d bloggers like this: